Documente Academic
Documente Profesional
Documente Cultură
www.fiascopress.org
Fiasco Press
www.fiascopress.org
a cluster of kites into the sky. Have a shot now at their tangles. Ill weigh them on a scale. The reward is quite dear. Im returning to my station and dropping my anchors, one off the stern and one off the prow. Your captain has been Nabahani, whos known the sea and fears no wave, nor any of its baleful associates.
Shaza
Ahmed Sheikh Nabahani
Wazami wa uziwani, wa mawimbi na miuya Muzamao zizimbwini, mahodari wa koweya Kwa kuwama na kwa tani, kubenuwa zenu ziya Nauza changu kimiya, kichatiya chashikani Nayuwa siwatanizi, hamugagwi yaweleya Yafumbuweni wayuzi, mutongowe moyamoya Kula aliye mfuzi, na nyundo huitumiya Kibafute natatiya, tatuwani watatuzi Welevu kitatuweni, munambiye nielewe Kuna kiwingu yangani, mvua itandaziwe Pepo husukuma pwani, nyunyu ni kama zijiwe Kwa kasi zitandushiwe, na kushukiya maini Hupenya ndani kwa ndani, ya uketo wa bahari Kama uzi sindanoni, upote pota hariri Yakashukiya shazani, na kufuma lulu duri Hapitwi na johari, nda kuu mno thamani Shaza lengetwe mtini, zizimbwini mwa nyongoza Haupo kitalaleni, haupati muwangaza Tandu hazionekani, yapokuwa zatepuza Si miti ya miujiza, yenezee duniyani Lulu ikikamilika, yuu la mti shazani
Fiasco Press
www.fiascopress.org
Dondole hukeketuka, ikatoka kiotoni Wimbini huisumbika, ikegesha ufuoni Yafumapo mkwambani, kitoche humemetuka Mianaza na miandi, eneo hungengezuka Huvuta kila mwenendi, kijopo hukusanyika Aipatao ni kandi, kashani akiiweka Wengi wametajirika, kwa ngandu na tu chandi Tatazi zingatatiya, mafundi zitatuweni Rajai naregezeya, kishada changu bwagani Nitawapa mwingi mwiya, fundo hili funguwani Niwapimiye kwa mani, tuzo tunu na hidaya Narejea kituoni, nanga zangu nazitiya Moya tezi na omoni, sambo ipate tuliya Nahudha ni Nabahani, bahari alozoweya Hachi shuu na miuya, wala wimbi uziwani
Fiasco Press
www.fiascopress.org